• HABARI MPYA

  Sunday, April 07, 2024

  AZAM FC YATINGA ROBÓ FAINALI KOMBE LA TFF


  WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kwenda Robó Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo Feisal Salum dakika ya kwanza, Ayoub Lyanga dakika ya 28 na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 69.
  Azam FC inakuwa timu ya sita kwenda Robó Fainali ya michuano hiyo baada ya Singida Black Stars, zamani Ihefu SC, Coastal Union, Namungo FC, Geita Gold na Tabora United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATINGA ROBÓ FAINALI KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top