• HABARI MPYA

  Sunday, April 07, 2024

  CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA SHEFFIELD UNITED 2-2 BRAMALL LANE


  BAO la dakika ya 90+3 la Oli McBurnie limewasaidia wenyeji, Sheffield United kupata sare ya 2-2 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Bramall Lane mjini Sheffield.
  Chelsea ilikuwa inaongoza 2-1, mabao yake yakifungwa na Thiago Silva dakika ya 11 na Chukwunonso Madueke dakika ya 66 dhidi ya bao la Sheffield United lililofungwa na Jayden Bogle dakika ya 32.
  Kwa sare hiyo, Chelsea inafikisha pointi 44 katika mchezo wa 31 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Sheffield United inabaki na pointi zake 16 za mechi 31 mkiani mwa Ligi, nafasi ya 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA SHEFFIELD UNITED 2-2 BRAMALL LANE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top