• HABARI MPYA

  Tuesday, April 16, 2024

  COLE PALMER APIGA NNE CHELSEA YAITANDIKA EVERTON 6-0 STAMFORD BRIDGE


  WENYEJI, Chelsea jana wameibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Ilikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji kinda wa miaka 21 wa Kimataifa wa England, Cole Jermaine Palmer aliyefunga mabao manne peke yake na kumfikia Mnorway wa Manchester City, Erling Haaland kileleni mwa mbio za Kiatu cha Dhahabu kila akiwa amefunga mabao 20 hadi sasa msimu huu.
  Palmer akifunga mabao yake dakika za 13, 18, 29 na la penalti dakika ya 64, huku mengine yakifungwa na mshambuliaji kinda wa miaka 22, Msenegal Nicolas Jackson dakika ya 44 na beki kinda wa miaka 20, Muingereza Alfie Gilchrist dakika ya 90.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 47 katika mchezo wa 31, ingawa inabaki nafasi ya tisa, wakati Everton inabaki na pointi zake 27 za mechi 32 nafasi ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COLE PALMER APIGA NNE CHELSEA YAITANDIKA EVERTON 6-0 STAMFORD BRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top