TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee la Tanzania Prisons katika mchezo huo wa leo wa ugenini, mshambuliaji George Enock Mpole Mwaigomole aliyetikisa nyavu za wapinzani dakika ya 45’+1.
Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 26 na kusogea nafasi ya 14 kutoka ya 15 kwenye ligi ya timu 16, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 38 za mechi nafasi ya sita baada ya timu hizo zote kucheza mechi 27.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment