• HABARI MPYA

  Tuesday, April 16, 2024

  KMC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0 PALE PALE MANUNGU KAZI YA SALIBOKO


  BAO pekee la Daruwesh Saliboko dakika ya 54 limeipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 32 katika mchezo wa 23 na kusogea nafasi ya tano ikizidiwa pointi moja na Coastal Unión ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 17 za mechi 22 sasa nafasi ya mwisho kwenye ligi ya timu 16.
  Timu mbili zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0 PALE PALE MANUNGU KAZI YA SALIBOKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top