• HABARI MPYA

  Monday, April 22, 2024

  ESPERANCE YAICHAPA MAMELODI 1-0, MAZEMBE 0-0 NA AHLY LUBUMBASHI


  WENYEJI, Espérance Sportive de Tunis juzi waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Olimpiki Hammadi Agrebi Jijini Radès.
  Bao pekee la Espérance Sportive de Tunis lilifungwa na mshambuliaji wake hatari, Mbrazil, Yan Medeiros Sasse dakika ya 41  baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Mamelodi Sundowns waliodhani amezidi na kumchambua kipa Ronwen Hayden Williams.
  Katika mchezo uliotangulia juzi jioni Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, wenyeji TP Mazembe walilazimishwa sare ya bila mabao na mabingwa watetezi, Al Ahly Misri.
  Timu hizo zitarudiana Ijumaa ijayo ya Aprili 26 na washindi wa jumla watakutana katika Fainali Mei 18 na Mei 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ESPERANCE YAICHAPA MAMELODI 1-0, MAZEMBE 0-0 NA AHLY LUBUMBASHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top