• HABARI MPYA

  Thursday, April 18, 2024

  IHEFU NA SINGIDA FOUNTAIN GATE ZATOSHANA NGUVU, 1-1 LITI


  TIMU ya Ihefu SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Kiungo Mghana, Nicholas Gyan anayeweza kucheza nafasi za ulinzi na ushambuliaji pia alianza kuifungia Singida Fountain Gate dakika ya 20, kabla ya kiungo mzawa, Joseph Mahundi kuisawazishia Ihefu SC dakika ya 70.
  Kwa matokeo hayo, Ihefu SC ambayo imebadilishwa jina na kuwa Singida Black Stars inafikisha pointi 25, ingawa inabaki nafasi ya 11 ikizidiwa tu wastani wa mabao na Singida Fountain Gate baada ya wote kucheza mechi 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU NA SINGIDA FOUNTAIN GATE ZATOSHANA NGUVU, 1-1 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top