• HABARI MPYA

  Thursday, April 18, 2024

  REAL MADRID YAING’OA MAN CITY KWA MATUTA ETIHAD


  TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa penalti 4-3 dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City kufuatia 
  sare ya 1-1 usiku huu Uwanja wa Jijini Etihad Jijini Manchester.
  Dakika 120 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, mshambuliaji Mbrazil, Rodrigo Silva de Goes akianza kuifungia Real Madrid dakika ya 12, kabla ya kiungo Mbelgiji, Kevin De Bruyne kuisawazishia Manchester City dakika ya 76.
  Matokeo hayo yakafanya sare ya jumla 4-4 kufuatia Real Madrid nayo kulazimishwa sare ya 3-3 nyumbani.
  Baada ya dakika 120, kwenye mikwaju ya penalti waliofunga za Real Madrid ni Jude Bellingham, Lucas Vázquez, José Ignacio Fernández ‘Nacho’ na Antonio Rüdiger, wakati Luka Modrić pekee alikosa.
  Waliofunga za Manchester City ni Julián Álvarez, Philip Foden na Ederson Santana de Moraes, huku Bernardo Silva na Mateo Kovačić wakikosa. 
  Sasa Real Madird itakutana na Bayern Munich ambayo imeitoa Arsenal.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAING’OA MAN CITY KWA MATUTA ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top