• HABARI MPYA

  Sunday, April 28, 2024

  SIMBA SC YAMFUKUZA KOCHA BENCHIKA BAADA YA MIEZI MITANO KAZINI


  KLABU ya Simba imetangaza rasmi kuachana na Kocha wake Mualgeria Abdelhak Benchikha baada ya miezi mitano tu tangu ajiunge na Wekundu hao wa Msimbazi.
  Simba inaachana na Benchika siku moja tu tangu Mualgeria huyo aiwezeshe kutwaa Kombe la Muungano kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jana usiku Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Aliwasili mwishoni mwa mwezi Novemba akasaini mkataba wa miaka miwili Novemba 28 kabla ya kuiwezesha timu kufika Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambako ilitolewa na mabingwa watetezi, Al Ahly.
  Lakini Simba ikatolewa katika Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ya ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup kwa penalti 6-5 na wenyeji, Mashujaa kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Na kwenye Ligi Kuu hadi sasa Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 za mechi 21, nyuma ya Azam FC yenye pointi 54 na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 62 baada ya timu zote kucheza mechi 24.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMFUKUZA KOCHA BENCHIKA BAADA YA MIEZI MITANO KAZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top