• HABARI MPYA

  Saturday, April 13, 2024

  GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA MTIBWA SUGAR NYANKUMBU


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Yussuf Mhilu dakika ya 20 na Valentino Mashaka dakika ya 35, wakati ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Jimson Mwanuke dakika ya 15 na Omary Ally dakika ya 77.
  Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 22 na kusogea nafasi ya 12, wakati Mtibwa Sugar inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 ikibaki na pointi zake 16 za mechi 21.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka na mbili zitamenyana baina yao nyumbani na ugenini kuwania kubaki Ligi Kuu, wakati itakayofungwa itakwenda kujaribu tena kujinusurukwa kucheza na timu ya Championship.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA MTIBWA SUGAR NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top