• HABARI MPYA

  Saturday, April 27, 2024

  LIVERPOOL YATOA DROO 2-2 NA WEST HAM UNITED LONDON


  MATUMAINI ya Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England yamezidi kufifia baada ya leo kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji, West Ham United Uwanja wa London  Jijni London.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na beki Mscotland, Andrew Henry Robertson dakika ya 48 na lingine akijfunga kipa Mfaransa, Alphonse Francis Areola dakika ya 65, wakati ya West Ham yamefungwa na beki Muingereza, Jarrod Bowen dakika ya 43 na mshambuliaji Mjamaica, Michail Antonio dakika ya 77. 
  Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 75 katika mchezo wa 35 na inabaki nafasi ya tatu, nyuma ya vinara Arsenal wenye pointi 77 za mechi 34 na mabingwa watetezi wenye pointi 76 za mechi 33, wakati West Ham inafikisha pointi 49 katika mchezo wa 35 nafasi ya nane.
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATOA DROO 2-2 NA WEST HAM UNITED LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top