• HABARI MPYA

    Wednesday, April 10, 2024

    SIMBA SC WASALI EID KIGOMA BAADA YA KIPIGO CHA MASHUJAA JANA


    MSHAMBULIAJI Mgambia wa Simba SC, Pa Omar Jobe akielekea msikitini kwa sala ya Eid El Fitri leo mjini Kigoma siku moja baada ya kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wenyeji, Mashujaa FC jana Uwanja wa Lake Tanganyika.
    Simba jana ilifungwa na wenyeji, Mashujaa FC kwa penalti 6-5 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90 jioni ya Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
    Mashujaa walitangulia kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake Reliant Rusajo dakika ya tano akimalizia pasi ya 60 Omar Omar, kabla ya mshambuliaji Muivory Coast , Freddy Koubalan kuisawazishia Simba dakika ya 51 akimalizia kazi nzuri ya Kibu Dennis.
    Mashujaa ilimaliza pungufu baada ya kiungo wake Said Juma ‘Makapu’ kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45+2.
    Kipa wa zamani wa Yanga, Eric Johola ndiye aliyeibuka shujaa kwa kupangua penalti mbili za Simba zilizopigwa na viungo, Mcameroon Leandre Willy Essomba Onana na Mmali, Sadio Kanoute.
    Waliofunga penalti za Mashujaa ni Sansón Madeleke, Michael Masinda, Idrisa Stambuli, Adam Adam, Mpoki Mwakinyuke na Baraka Mtui, huku Zuberi Dabi pekee akikosa.
    Kwa upande wa Simba waliofunga ni Nahodha Mohamed Hussein 'Tshabalala', Israel Mwenda, Freddy Koublan, Muzamil Yassin na Ladack Chasambi.
    GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WASALI EID KIGOMA BAADA YA KIPIGO CHA MASHUJAA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top