• HABARI MPYA

  Thursday, April 25, 2024

  LIVERPOOL UBINGWA HAUWATAKI, WATANDIKWA 2-0 NA EVERTON


  WENYEJI, Everton wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao,  Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Goodison Park, Liverpool.
  Mabao yaliyoikata kilimi Liverpool yamefumgwa na Waingereza, beki Jarrad Branthwaite dakika ya 27 na mshambuliaji Dominic Calvert-Lewin dakika ya 58.
  Kwa ushindi huo, Everton inafikisha pointi 33 na kusogea nafasi ya 16, wakati Liverpool inabaki na pointi zake 74 nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na Arsenal baada ya wote kucheza mechi 34.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL UBINGWA HAUWATAKI, WATANDIKWA 2-0 NA EVERTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top