• HABARI MPYA

  Monday, April 15, 2024

  LAKRED AREJEA, SIMBA KUWEKA KAMBI ZANZIBAR DHIDI YA YANGA


  KIPA wa Simba, Ayoub LAkred amerejea na kuanza mazoezi leo Uwanja wa MO Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya watani, Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini.
  Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kwamba Lekred alikwenda kwao, Morocco baada ya mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Al Ahly Jijini Cairo nchini Misri Aprili 5, mwaka huu kwa sababu ya matatizo ya kifamilia.
  Aidha, Ahmed Ally amesema kikosi kitaondoka mapema kesho kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LAKRED AREJEA, SIMBA KUWEKA KAMBI ZANZIBAR DHIDI YA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top