• HABARI MPYA

    Thursday, June 18, 2026

    TEGISI MOMANYI APIGA HAT-TRICK PAMBA YAICHAPA MTIBWA 4-0 MWANZA


    TIMU ya Pamba Jiji FC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
    Ilikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji Mathew Tegisi Momanyi aliyefunga mabao matatu dakika za 18, 46 na 49, huku bao linguine likifungwa na Mkenya mwenzake, mshambuliaji pia Shaphan Siwa dakika ya 44.
    Kwa ushindi huo mnono, Pamba Jiji FC inafikisha pointi 36, ingawa inabaki nafasi ya saba na Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 27 nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16 baada ya timu hizo zote kucheza mechi 27.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TEGISI MOMANYI APIGA HAT-TRICK PAMBA YAICHAPA MTIBWA 4-0 MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top