• HABARI MPYA

  Sunday, April 28, 2024

  HATIMAYE PAMBA FC YAREJEA LIGI KUU, BIASHARA NA MBEYA KWANZA KUJARIBU ‘MLANGO WA UANI’


  HATIMAYE timu ya Pamba ya Mwanza imefanikiwa kurejea Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mbuni FC leo katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya NBC Championship Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Ushindi huo unaifanya Pamba FC imalize Ligi ya NBC Championship na pointi 67, nyuma ya mabingwa, Ken Gold ya Mbeya iliyomaliza na pointi 70 na wote wanapanda Ligi Kuu moja kwa moja.
  Timu ya Mbeya Kwanza ya Mbeya inayotumia Uwanja wa Nangwanda Sijaona wa Mtwara iliyomaliza na pointi 65 nafasi ya tatu itamenyana na Biashara United ya Mara iliyomaliza na pointi 62 na mshindi wa jumla atakwenda kumenyana na timu iliyoporomoka kutoka Ligi Kuu kujaribu kupanda kupitia mchujo huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HATIMAYE PAMBA FC YAREJEA LIGI KUU, BIASHARA NA MBEYA KWANZA KUJARIBU ‘MLANGO WA UANI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top