• HABARI MPYA

  Wednesday, April 17, 2024

  AZAM FC YABANWA MBAVU NA MASHUJAA CHAMAZI, NGOMA DROO 0-0


  WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya bila mabao na Mashujaa katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 51 katika mchezo wa 23 na inabaki nafasi ya pili ikizidwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao Mashujaa FC ya Kigoma baada ya sare ya leo wanafikisha pointi 22 katika mchezo wa 23 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16 ikiizidi tu wastani wa mabao Tabora United waliyopanda Ligi Kuu msimu huu pamoja na JKT Tanzania.
  Kwa ujumla hali si shwari kwa timu zote zilizopanda msimu huu, kwani JKT Tanzania nayo inashika nafasi ya  13 ikiwa na pointi 22 pia za mechi 22, wakati mabingwa mara mbili mfululizo, 1999 na 2000, Mtibwa Sugar wanashika mkia wakiwa na pointi 17 za mechi 22.
  Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YABANWA MBAVU NA MASHUJAA CHAMAZI, NGOMA DROO 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top