• HABARI MPYA

  Sunday, April 14, 2024

  GUEDE APIGA MBILI, KI MOJA YANGA YASHINDA 3-0 KIRUMBA


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mabao ya Yanga SC yamefungwa na mshambuliaji wake Muivory Coast, Joseph Guédé Gnadou mawili, dakika ya 42 na 69, huku lingine likifungwa na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 66.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 55 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi nane zaidi ya Azam FC baada ya wote kucheza mechi 21.
  Kwa upande wao Singida Fountain Gate baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 24 za mechi 22 sasa wakishuka kwa nafasi moja hadi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GUEDE APIGA MBILI, KI MOJA YANGA YASHINDA 3-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top