• HABARI MPYA

  Sunday, April 21, 2024

  KEN GOLD YAPANDA LIGI KUU, PAMBA NI SUALA LA MUDA TU


  TIMU ya Ken Gold ya Mbeya imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate Talents leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Kwa ushindi huo, Ken Gold inafikisha pointi 67 katika mchezo wa 29 ambazo ni Pamba pekee inaweza kuzifikisha kama itashinda mechi yake ya mwisho na kwa sababu timu za kupanda Ligi Kuu ni mbili kutoka Championship imekwishajihakikishia kupanda.
  Pamba FC baada ya ushindi wa 2-1 leo dhidi ya TMA leo Uwanja wa Black Rhino Academy mjini Karatu imefikisha pointi 64 na inahitaji ushindi katika mchezo wa mwisho kujihakikishia kurejea Ligi Kuu.
  Mbeya Kwanza nayo baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Greem Warriors leo Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara imefikisha pointi 62 na itahitaji ushindi kwenye mechi ya mwisho kuangalia uwezekano wa kurejea Ligi Kuu kama Pamba itapoteza mechi ya mwisho.
  Biashara United baada ya kufungwa 2-1 na Pan African leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo huko Mbweni na sasa inaweza kurejea Ligi Kuu kupitia mchujo (PlayOffs) pekee.
  Wakati timu mbili za kwanza zitapanda moja kwa moja, zitakazomaliza nafasi ya tatu na ya nne zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atakwenda kucheza na timu iliyoporomoka kutoka Ligi Kuu kujaribu kupanda.
  Timu mbili mwisho zitashuka moja kwa moja na nne zitamenyana katika mchujo wa kujaribu kuepuka kushuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KEN GOLD YAPANDA LIGI KUU, PAMBA NI SUALA LA MUDA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top