• HABARI MPYA

  Wednesday, April 24, 2024

  FREDDY MICHAEL KOUBLAN AIPELEKA SIMBA FAINALI MUUNGANO CUP


  TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, KVZ katika mchezo wa Nusu Fainali ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mabao ya Simba SC yalifungwa na mshambuliaji Muivory Coast, Freddy Michael Koublan dakika ya 25 na beki Israel Patrick Mwenda dakika ya 90’+5 kwa penalti.
  Katika Fainali ya michuano hiyo inayorejea baada ya miaka 20, Simba SC watakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho baina ya KMKM na Azam FC.
  Fainali itafanyika Jumapili na mechi zote zitapigwa Uwanja wa New Amaan Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FREDDY MICHAEL KOUBLAN AIPELEKA SIMBA FAINALI MUUNGANO CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top