• HABARI MPYA

  Sunday, April 07, 2024

  SALAH AINUSURU LIVERPOOL KUPIGWA NA MAN UNITED


  WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Winga Mcolombia, Luis Díaz aliifungia bao la kuongoza Liverpool dakika ya 23, kabla ya Manchester United kutoka nyuma kwa mabao ya kiungo Mreno Bruno Fernandes dakika ya 50 na mshambuliaji ‘bwana mdogo’ wa miaka 18, Muingereza mwenye asili ya Ghana, Kobbie Boateng Mainoo dakika ya 67.
  Mshambuliaji Mmisri, Mohamed Salah akaisawazishia Liverpool dakika ya 84 kwa penalti kufuatia beki Muingereza mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Aaron Wan-Bissaka kumchezea rafu kiungo Muingereza, Harvey Elliott.
  Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 71, ingawa inabaki nafasi ya pili, ilizidiwa tu wastani wa mabao na Arsenal na wote wakiwa mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 70 kufuatia timu zote kucheza mechi 31.
  Kwa upande wao Manchester United baada ya sare ya leo wanafikisha pointi 49 katika mchezo wa 31 pia nafasi ya sita wakizidiwa pointi nane na Tottenham Hotspur yenye mechi moja mkononi pia katika nafasi ya tano, wote wakiwa nyuma ya Aston Villa yenye pointi 60 za mechi 32.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH AINUSURU LIVERPOOL KUPIGWA NA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top