• HABARI MPYA

  Monday, April 15, 2024

  YANGA NA NBC WAZINDUA KADI ZA KIMATAIFA ZA UANACHAMA


  BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Mabingwa wa kihistoria Young Africans Sports Club tumezindua kadi za kimataifa za uanachama wa Klabu inayofahamika kama ‘NBC Yanga Membership Card’.
  Hatua hii kwa pamoja na faida nyingine inalenga kurahisisha malipo ya uanachama kwa wanachama wa Young Africans na hivyo kusaidia kuongeza mapato ya Klabu yetu.
  Hafla ya uzinduzi wa kadi hizo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi iliyohusisha viongozi waandamizi wa pande zote mbili, wafanyakazi benki ya NBC, wanachama na mashabiki mashuhuri wa Young Africans SC
  Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Bw. Steven Mguto alimuwakilisha Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia.
  Kadi hii tunayoizindua leo, imeambatana na faida nyingi ambazo Wanachama wa Young Africans watanufaika nazo ikiwemo urahisi wa kununua tiketi za mechi za NBC Premier League, FA na CAF Champions League kwa mfumo wa N-Card. Wananchi sasa hatuhitaji tena kununua N-Card kwa kuwa kadi hizi tayari zimeunganishwa na mfumo wa N-Card. Kadi hii pia inaweza kutumika kufanya malipo katika vituo vyote vya TEMESA nchini ikiwemo malipo ya huduma ya Ferry -Kigamboni.’’ Mkurugenzi wa Biashara. Bw. Elvis Ndunguru.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA NBC WAZINDUA KADI ZA KIMATAIFA ZA UANACHAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top