• HABARI MPYA

  Wednesday, April 24, 2024

  ARAJIGA AIFUATA SIMBA SC KOMBE LA MUUNGANO ZANZIBAR


  REFA Ahmed Arajiga wa Manyara ni miongoni mwa waamuzi watatu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara walioteuliwa kuchezesha Kombe la Muungnao, michuano inayotarajiwa kuanza leo usiku Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Wengine kutoka Bara ni Frank John Komba na Amina Samuel Kyando wakati wa Ligi Kuu ya PBZ Zanzíbar ni wanne, Al Ahmada Mbwana, Ali Ramadhani Ibada, Nasir Siyah ‘Msomali’ na Mohamed Simba Khamis.
  Simba itafungua dimba Kombe la Muungano michuano inayorejea baada ya miaka 20 kwa kumenyana na wenyeji, KVZ katika Nusu Fainali leo kuanzia Saa 2:15 usiku Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar wakati Azam FC kesho Azam FC itaumana na KMKM.
  Washindi wa mechi za Nusu Fainali watakutana katika Fainali Aprili 27 hapo hapo Amaan Complex.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARAJIGA AIFUATA SIMBA SC KOMBE LA MUUNGANO ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top