• HABARI MPYA

  Friday, April 26, 2024

  MAN CITY YAICHAPA 4-0 BRIGHTON & HOVE ALBION


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Brighton & Hove Albion Uwanja wa The Amex, Falmer, East Sussex.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na kiungo mkongwe Mbelgiji, Kevin De Bruyne dakika ya 17 na washambuliaji Muingereza, Philip Foden mawili dakika ya 26 na 34 na' Muargentina, Julián Álvarez dakika ya 62.
  Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 76 katika mchezo wa 33 ikizidiwa pointi moja na vinara, Arsenal ambao pia wamecheza mechi moja zaidi, wakati Brighton & Hove Albion inafikisha pointi 44 katika mchezo wa 33 nafasi ya 11.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAICHAPA 4-0 BRIGHTON & HOVE ALBION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top