• HABARI MPYA

  Sunday, April 21, 2024

  LIVERPOOL YAICHAPA FULHAM 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA


  TIMU ya Liverpool imefufua matumaini ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham FC leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na beki Muingereza Trent Alexander-Arnold dakika ya 32, kiungo Mholanzi Ryan Gravenberch dakika ya 53 na mshambuliaji Mreno Diogo Jota dakika ya 73, wakati bao pekee la Fulham FC limefungwa na beki Mbelgiji, Timothy Castagne dakika ya  45'+2.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 74 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na Arsenal baada ya wote kucheza mechi 33, wakati Fulham inabaki na pointi zake 42 za mechi 34 nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA FULHAM 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top