• HABARI MPYA

  Saturday, April 13, 2024

  MAN UNITED YAGAWANA POINTI NA BOURNEMOUTH


  TIMU ya Manchester United imetoa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji, AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vitality mjini Bournemouth, Dorset.
  Mabao yote ya Manchester United yamefungwa na kiungo Mreno, Bruno Fernandes dakika ya 31 na la penalti dakika ya 65, wakati ya AFC Bournemouth yamefungwa na mshambuliaji Muingereza, Dominic Solanke dakika ya 16 na Mholanzi, Justin Dean Kluivert dakika ya 36.
  Kwa matokeo hayo, Manchester United inafikisha pointi 50 nafasi ya saba, wakati AFC Bournemouth inafikisha pointi 42 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 32
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAGAWANA POINTI NA BOURNEMOUTH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top