• HABARI MPYA

  Thursday, April 25, 2024

  SIMBA QUEENS YAIKANYAGA YANGA PRINCES 3-1 CHAMAZI


  TIMU ya Simba Queens imeendeleza ubabe kwa watani wao, Yanga Princess baada ya kuwachapa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba Queens leo yamefungwa na kiungo Aisha Juma Mnunka mawili dakika ya 49 na 90’+2 na mshambuliaji Mkenya, Jentrix Shikangwa Milimu dakika ya 66, wakati bao pekee la Yanga Princess limefungwa na kiungo Mmarekani, Kaeda Wilson dakika ya 90’+5.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YAIKANYAGA YANGA PRINCES 3-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top