• HABARI MPYA

    Wednesday, December 27, 2023

    ZANZIBAR HEROES NA BARA HAKUNA MBABE, 0-0 AMAAN


    TIMU za taifa ya Tanzania Bara na Zanzibar leo zimetoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa maalum wa kirafiki kwa ajili ya kuufungua Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Katika mchezo huo uliohuhudhuriwa na Rais wa awamu ya nane, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, timu zote zilishambuliana kwa zamu.
    Baada ya mchezo huo, Kocha Mualgeria, Adel Amrouche atateua wachezaji 27 kuunda kikosi cha mwisho cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachokwenda kambini kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwakani nchini Ivory Coast.
    Hata hivyo ni wachezaji 23 tu ndio watakaoruhusiwa kucheza Fainali za AFCON zitakazofanyika kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 mwakani nchini Ivory Coast.
    Taifa Stars imepangwa Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
    Kwa Taifa Stars hizo Zita kuwa Fainali za tatu za AFCON kucheza baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri, kote wakitolewa hatua ya makundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZANZIBAR HEROES NA BARA HAKUNA MBABE, 0-0 AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top