• HABARI MPYA

  Thursday, December 07, 2023

  TWIGA STARS WAPATA MAPOKEZI MAZURI BAADA YA KUFUZU WAFCON


  KIKOSI cha timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ kimepata mapokezi mazuri kilipowasili Alfajiri ya leo kutoka Lome nchini Togo ambako kilifanikiwa kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) mwakani nchini Morocco.
  Mapokezi ya Twiga Stars Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam yaliongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro ambaye aliwapongeza mabinti hao kwa mafanikio hayo.
  VIDEO: WAZIRI DK DAMAS NDUMBARO AKIWAPONGEZA TWIGA STARS LEO
  Twiga Stars inayofundishwa na kocha mzalendo, Bakari Nyundo Shime imefanikiwa kufuzu WAFCON 2024 Morocco licha ya kufungwa 2-0 na wenyeji, Togo juzi Uwanja wa Kegue Jijini Lome.
  Katika mchezo huo marudiano Raundi ya Pili na ya mwisho ya kufuzu mabao yote ya Togo yalipatikana dakika 15 za mwisho na kwa matokeo hayo Twiga Stars inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2, kufuatia kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam Alhamisi iliyopita.
  Mabao ya Twiga Stars katika mchezo wa kwanza Twiga Stars uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam yalifungwa na mshambuliaji wa Besiktas ya Uturuki, Opa Clement mawili, dakika ya 45 na ushei kwa penalti na dakika ya 81, huku lingine Yawa Konou wa Togo akijifunga dakika ya 57.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS WAPATA MAPOKEZI MAZURI BAADA YA KUFUZU WAFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top