• HABARI MPYA

  Thursday, December 14, 2023

  DODOMA JIJI YAICHAPA MAGEREZA DAR 1-0 ASFC NA KUSONGA MBELE


  BAO pekee la Hassan Mwaterema limeipa Dodoma Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Magereza ya Dar es Salaam katika mchezo wa hatua ya 64 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mechi nyingine za leo ASC JKT Tanzania imeitoa Kurugenzi ya Simiyu kwa mabao 5-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam, Ihefu SC imeitoa Rospa FC ya Mtwara kwa kuichapa mabao 3-0 Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya na Coastal Unión imeichapa Greenland ya Kagera mabao 2-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA MAGEREZA DAR 1-0 ASFC NA KUSONGA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top