• HABARI MPYA

  Thursday, December 07, 2023

  FAINALI ZA NBA IN-SEASON TOURNAMENT KUPIGWA T-MOBLE ARENA


  UKUMBI wa T-Mobile Arena uliopo Las Vegas ndio uta-host Fainali za michuano mpya ya NBA In-Season Tournament inayofanyika kwa mara kwa kwanza kabisa huku timu zitakazomenyana zikifanya mazoezi siku ya Jumatano.
  Nusu fainali itafanyika Alhamisi kuamkia Ijumaa, Indiana Pacers wakimenyana na Milwaukee Bucks kabla ya New Orleans Pelicans kumenyana na Los Angeles Lakers – na washindi wa mechi hizo watakutana Jumamosi kuamkia Jumapili katika Fainali katika michuano hiyo yenye fedha nyingi kwa washindi.
  Wachezaji wote wa timu zilizofika Nusu Fainali ambao wana mikataba watapata $100,000 USD na wale wenye mikataba maalum watapata nusu yake kila mmoja.
  Wkifika Fainali dau litapanda hadi $200,000 na $500,000 kila mmoja kwa timu itakayotwaa taji hilo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FAINALI ZA NBA IN-SEASON TOURNAMENT KUPIGWA T-MOBLE ARENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top