• HABARI MPYA

  Friday, December 08, 2023

  IHEFU SC YAZINDUKA NA KUITANDIKA TABORA UNITED 2-1 MBARALI


  TIMU ya Ihefu SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tabora United katik mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.
  Mabao ya Ihefu SC yote yamefungwa na beki Vedastus Mwihambi dakika ya 40 na 56, wakati la Tabora United limefungwa na beki Mkongo Andy Bikoko dakika ya 84.
  Kwa ushindi huo, Ihefu SC inafikisha pointi 13 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya 13, wakati Tabita United inabaki na pointi zake 15 za mechi 12 nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YAZINDUKA NA KUITANDIKA TABORA UNITED 2-1 MBARALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top