• HABARI MPYA

    Monday, December 18, 2023

    MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA AKIDA MAKUNDA, NYOTA WA ZAMANI YANGA

    AKIDA MOHAMED MAKUNDA
    ALIZALIWA Julai 13, mwaka 1974 huko Moshi mkoani Kilimanjaro, kabla ya familia yake kuhamia Tanga ambako alisoma shule ya Msingi Mwakizaro hadi darasa la Tano, akarejea Moshi ambako alimalizia hadi darasa la Saba katika Shule ya Karanga.
    Soka alianzia Tanga katika timu za watoto za Chumbageni, Kigwere na Mtupie na aliporejea Moshi alichezea timu ya watoto ya Soweto, kabla ya kuhamia Dar es Salaam ambako alicheza timu za Vita ya Kinondoni na Forest ya Ilala, iliyomfanya awavutie Pan Africans waliomsajili mwaka 1994.
    Msimu mmoja wa kuwa na Pan Africans ulimfanya awavutie vigogo, Simba SC waliomsajili mwaka 1996 ambako alicheza kwa msimu mmoja kabla ya kuhamia kwa watani, Yanga mwaka 1997.
    Alicheza Yanga misimu mitatu hadi mwaka 1999 alipokwenda Falme za Kiarabu kujiunga na klabu ya Daraja la Pili, Al Hamriya ambako alicheza hadi mwaka 2001 aliporejea nyumbani na kuamua kuachana na soka moja kwa moja.
    Alikuwepo kwenye kikosi cha Yanga kilichofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998 kwa mara ya kwanza ikiwa timu ya kwanza ya Tanzania kufika hatua hiyo. 
    Ni mtoto wa beki tatu wa zamani wa Coastal Union ya Tanga, Mohamed Makunda miaka ya 1970 – ambaye amecheza pia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuanzia mwaka 1995 hadi 1999 na sasa akiwa ana umri wa miaka 49 tu ni baba wa familia na anajishughulisha na biashara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA AKIDA MAKUNDA, NYOTA WA ZAMANI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top