• HABARI MPYA

  Wednesday, December 13, 2023

  ARSENAL YAMALIZA KIBABE KUNDI A BAADA YA SARE YA UGENINI


  TIMU ya Arsenal imemaliza kileleni mwa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya sare ya 1-1 na PSV usiku wa jana Uwanja wa Philips Stadion Jijini Eindhoven nchini Uholanzi.
  Arsenal ilitangulia na bao la Eddie Nketiah dakika ya 42, kabla ya mshambuliaji Mbelgiji Yorbe Vertessen dakika ya 50.
  Kwa matokeo hayo, Arsenal inamaliza na pointi 13, ikifuatiwa na PSV pointi tisa na zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora, wakati Lena iliyomaliza na pointi nane baada ya kuifunga 2-1 Sevilla ya Hispania nyumbani Ufaransa jana inakwenda Europa League.
  Sevilla safari yake kwenye michuano ya msimu huu imeishia hapa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAMALIZA KIBABE KUNDI A BAADA YA SARE YA UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top