• HABARI MPYA

  Wednesday, December 06, 2023

  ARSENAL YASHINDA MECHI DUME 4-3 DHIDI YA LUTON TOWN UGENINI


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya wenyeji, Luton Town katika mchezo mkali na wa kusisimua wa Ligi Kuu ya England usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Kenilworth Road mjini Luton, Bedfordshire.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Martinelli dakika ya 20, Gabriel Jesus dakika ya 45, 0' Kai Havertz dakika ya 60 na Declan Rice  dakika ya 90.
  Kwa upande wao, Luton Town mabao yao yamefungwa na Gabriel Osho dakika ya 25, Elijah Adebayo dakika ya 49 na Ross Barkley dakika ya 57.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 36 katika mchezo wa 15 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tano zaidi ya Liverpool na sita zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao wote wamecheza mechi 14, wakati Luton Town inabaki na pointi zake tisa za mechi 15 nafasi ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YASHINDA MECHI DUME 4-3 DHIDI YA LUTON TOWN UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top