• HABARI MPYA

  Friday, December 08, 2023

  PACOME MCHEZAJI BORA WA YANGA MWEZI NOVEMBA


  KIUNGO Muivory Coast wa Yanga, Peodoh Pacôme Zouzoua (30) ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa klabu hiyo kwa mwezi Novemba, mwaka huu.
  Pacome amengakua Tuzo hiyo kwa kuwapiku kiungo Mganda, Khalid Aucho (30) na mshambuliaji chipukizi mzawa, Clement John Mzize au Walid (19) alioingia nao Fainali. 
  Kwa ushindi huo, Pacome atazawadiwa Fedha taslimu Sh. Milioni 4 kutoka kwa wadhamini, NIC Insurance mara tu atakaporejea kutoka Ghana ambako amesafiri timu kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Medeama SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PACOME MCHEZAJI BORA WA YANGA MWEZI NOVEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top