• HABARI MPYA

  Saturday, December 23, 2023

  YANGA YAITANDIKA SIMBA 4-0 LIGI YA VIJANA U20 CHAMAZI

  TIMU ya Yanga SC jana iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya watani wao, Simba SC katika mchezo wa Kundi A Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yalifungwa na Willyson Christopherdakika ya 16, Sheikhan Khamis dakika ya 23, Ahmed Fredrick dakika ya 47 na ushei na Ramadhan Hemed dakika ya 48.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya nne katika kundi la timu nane, ambalo Azam FC inaongoza kwa pointi zake 14, ikifuatiwa na Coastal Union yenye pointi 13 na Ihefu 11, wakati Simba inabaki na pointi zake tano mkiani baada ya wote kucbheza mechi saba.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAITANDIKA SIMBA 4-0 LIGI YA VIJANA U20 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top