• HABARI MPYA

  Thursday, December 21, 2023

  AZAM FC YAITANDIKA KAGERA SUGAR 4-0 PALE PALE KAITABA ZUBERI AOKOA PENALTI YA CHIRWA


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi ya NBC Tanzania Bara leo Uwanj wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo mzawa, Feisal Salum dakika ya tisa, mshambuliaji Mzimbabwe Prince Dube dakika ya 29, beki mzawa Pascal Msindo dakika ya 12  na mshambuliaji Msenegal, Alassan Diao dakika ya 84.
  Sifa kwake kipa mzawa, Zuberi Foba aliyeokoa mkwaju wa penalti wa mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya 49.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 13, ikiendelea kuongoza Ligi kwa pointi nne zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mechi tatu mkononi.
  Kagera Sugar baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 13 za mechi 13 nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAITANDIKA KAGERA SUGAR 4-0 PALE PALE KAITABA ZUBERI AOKOA PENALTI YA CHIRWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top