TIMU ya Azam FC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Al Hilal walitangulia kwa bao la mshambuliaji Mzambia, Albert Kangwanda dakika ya 27, kabla ya kiungo mzawa, Iddi Suleiman ‘Nado’ kuisawazishia Azam FC dakika ya 80.
0 comments:
Post a Comment