• HABARI MPYA

  Tuesday, December 26, 2023

  LIVERPOOL YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA BURNLEY 2-0 TURF MOOR


  TIMU ya Liverpool imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Burnley FC
  leo Uwanja wa Turf Moor mjini Burnley.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Darwin Núñez dakika ya sita na Diogo Jota dakika ya 90 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 42 katika mchezo wa 19 na kupanda tena kileleni mwa Ligi Kuu wakiizidi Arsenal pointi mbili, ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Burnley wanabaki na pointi zao 11 za mechi 19 sasa katika nafasi y 19 kwenye Ligi y timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitateremka hadi Ligi ya Championship.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA BURNLEY 2-0 TURF MOOR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top