• HABARI MPYA

  Thursday, December 21, 2023

  GEITA GOLD YAIBAMIZA SINGIDA BIG STARS 1-0 NYANKUMBU


  WENYEJI, Geita Gold wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.
  Bao pekee la Geita Gold limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo kwa sasa, Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 79 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 16 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya 10, wakati Singida wanabaki na pointi zao 20 za mechi 14 sasa nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAIBAMIZA SINGIDA BIG STARS 1-0 NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top