• HABARI MPYA

  Sunday, December 17, 2023

  MAN UNITED PUNGUFU YAIKOMALIA LIVERPOOL ANFIELD, 0-0


  WENYEJI, Liverpool wamelazimishwa sare ya bila kufungana na mahasimu, Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Manchester United walimaliza pungufu mechi hiyo kufuatia beki wake Mreno, Diogo Dalot kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa mkupuo dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida za mchezo.
  Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 38 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Arsenal inayoongoza, wakati Manchester United inafikisha pointi 28 na kusogea nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED PUNGUFU YAIKOMALIA LIVERPOOL ANFIELD, 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top