• HABARI MPYA

  Thursday, December 21, 2023

  TANZANIA PRISONS NAMUNGO FC 1-0 SOKOINE


  TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Bao pekee la Tanzania Prisons leo limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Samson Baraka Mbangula dakika ya 42 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 17 na kusogea nafasi ya tisa wakizidiwa tu wastani wa mabao na Namungo FC inayoendelea kushika nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS NAMUNGO FC 1-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top