• HABARI MPYA

  Thursday, December 07, 2023

  YANGA SC INA SHUGHULI PEVU NA MEDEAMA KESHO UWANJA WA BABA YARA


  KIKOSI cha Yanga SC leo kimenya mazoezi ya mwisho kuuzoea Uwanja wa Baba Yara Jijini Kumasi nchini Ghana tayari kwa mchezo wake wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Medeama kesho Saa 1:00 usiku.
  Katika mechi zake mbili za mwanzo, Yanga ilifungwa 3-0 CR Belouizdad na Novemba 24 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers na sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Al Ahly Desemba 2 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa upande wao, Medeama mechi ya kwanza walichapwa 3-0 pia na Al Ahly Novemba 25 Jijini Cairo, kabla ya kushinda 2-1 nyumbani dhidi ya CR Belouizdad Desemba 1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC INA SHUGHULI PEVU NA MEDEAMA KESHO UWANJA WA BABA YARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top