• HABARI MPYA

  Saturday, December 30, 2023

  MABINGWA MLANDEGE SARE TENA, 1-1 NA VITAL’O KOMBE LA MAPINDUZI


  MABINGWA watetezi, Mlandege FC wamekamilisha mechi mbili za Kundi A bila ushindi baada ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Vital’O ya Burundi leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mlandege walitangulia kwa bao la kiungo Optatus Yustin Lupekenya dakika ya 45 baada ya kazi nzuri ya Mcolombia, Diego Fernando, lakini mshambuliaji Kessy Jordan Nimbona akaisawazishia Vital’O dakika ya 64.
  Timu zote sasa zina pointi mbili bada ya kutoa sare katika mechi zao za kwanza pia, Mlandege na Azam FC na Vital’O na Chipukizi United.
  Mechi nyingine ya Kundi A itafuatia Saa 2:15 kati ya Azam FC na Chipukizi United hapo hapo New Amaan Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABINGWA MLANDEGE SARE TENA, 1-1 NA VITAL’O KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top