• HABARI MPYA

  Wednesday, December 27, 2023

  MANCHESTER UNITED YATOKA NYUMA KWA MABAO MAWILI NA KUICHAPA ASTON VILLA 3-2


  TIMU ya Manchester United usiku wa jana imetoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda 3-2 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Aston Villa ilitangulia kwa mabao ya John McGinn dakika ya 21 na Leander Dendoncker dakika y 26, kabla ya Alejandro Garnacho kuisawazishia Manchester United kwa mabao mfululizo dakika ya 59 na 71 na Rasmus Hojlund kufunga la ushindi dakika ya 82.
  Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 31 na kusogea nafasi ya sita, wakati Aston Villa inabaki na pointi zake 39 nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER UNITED YATOKA NYUMA KWA MABAO MAWILI NA KUICHAPA ASTON VILLA 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top