• HABARI MPYA

  Sunday, December 10, 2023

  MAN CITY YAZINDUKA, YAICHAPA LUTON TOWN 2-1


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameweka hai matumaini ya kutetea taji la Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Luton Town Uwanja wa Kenilworth Road mjini Luton, Bedfordshire.
  Haukuwa ushindi mwepesi, kwani ilibidi Manchester City watoke nyuma baada ya Elijah Adebayo kuanza kuifungia Luton Town dakika ya 45 na ushei.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Bernardo Silva dakika ya 62 na Jack Grealish dakika ya 65 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 33, ingawa wanabaki nafasi ya nne nyuma ya Aston Villa pointi 35, Arsenal pointi 36 na Liverpool 37 baada ya wote kucheza mechi 16.
  Kwa upande wao Luton Town baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao tisa nafasi ya 18 baada ya kucheza mechi 16 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAZINDUKA, YAICHAPA LUTON TOWN 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top