• HABARI MPYA

    Saturday, December 09, 2023

    BOURNEMOUTH YAIMIMINIA MAN UNITED MABAO 3-0 OLD TRAFFORD


    TIMU ya Manchester United imechapwa mabao 3-0 na AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
    Mabao ya AFC Bournemouth yamefungwa na Dominic Solanke dakika ya tano, Philip Billing dakika ya 68 na Marcos Senesi dakika ya 73.
    Kwa ushindi huo, AFC Bournemouth inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya 13, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 27 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 16.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BOURNEMOUTH YAIMIMINIA MAN UNITED MABAO 3-0 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top