• HABARI MPYA

  Friday, December 08, 2023

  TANZANIA PRISONS YALIAMSHA DUDE, YAWAPIGA MASHUJAA 2-0 KIGOMA


  TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na kiungo Jumanne Elfadhili dakika ya 69 na mshambuliaji Jeremiah Juma dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons wanafikisha pointi 14 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya 10, wakati Mashujaa inabaki na pointi zake tisa za mechi 11 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YALIAMSHA DUDE, YAWAPIGA MASHUJAA 2-0 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top