• HABARI MPYA

  Saturday, December 09, 2023

  LIVERPOOL YAICHAPA CRYSTAL PALACE PUNGUFU 2-1 SELHURST PARK


  TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
  Crystal Palace ilitangulia kwa bao la Jean-Philippe Mateta dakika ya 57 kwa penalti, kabla ya Mohamed Salah kuisawazishia Liverpool dakika ya 76, hilo likiwa bao lake la 200 tangu ajiunge na Wekundu hao wa Anfield 
  Bao la ushindi la Liverpool limefungwa na Harvey Elliott dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao Crystal Palace walimaliza pungufu kufuatia Jordan Ayew kuonyeshwa kadi mbili za njano na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 75.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 16 na kupanda kileleni ikiizidi pointi moja Arsenal yenye mechi moja mkononi, wakati Crystal Palace inabaki na pointi 16 za mechi 16 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA CRYSTAL PALACE PUNGUFU 2-1 SELHURST PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top